This job listing has expired and may no longer be relevant!
22 Apr 2020

Career Opportunities at National Electoral Commission (Over 30+ Recommended Jobs Update)

Welcome to Jobweb Tanzania. This website helps you to achieve your career dream by linking you to vacancies from Top Companies in Tanzania. Job Seekers are also exposed to best articles for career growth and development. Click here to subscribe for job alerts We strongly advise graduates not to pay money before getting a Job. Report fraudulent jobs to [email protected]


  TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI  ZA MUDA

Kwa mujibu  wa kifungu cha 7A (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi , Sura ya 343 na kifungu cha 10(6) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa,Sura ya 292 kikisomwa pamoja na kanuni  ya 9 ya Kanuni za uboreshaji  wa Daftari  la Kudumu la Wapiga kura uchaguzi wa Rais  na wabunge  za mwaka 2018 na Kanuni ya  12 ya Kanuni za uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura , Uchaguzi wa Madiwani za mwaka 2018,Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea  anapenda kuwajulisha kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura  katika Jimbo la Peramiho linaanza hivi karibuni,Katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu  la Wapiga kura Vituoni ,watatumika  Waandishi wasaidizi  na BVR  Kit Operators

 • BVR Kit Operators  nafasi 16
 • Waandishi Wasaidizi nafasi 16

Hivyo anakaribisha maombi kutoka kwa watanzania wenye sifa  na uwezo  wa kujaza  nafasi hizo;

 • Sifa za Mwombaji  wa nafasi  ya BVR Kit Operator
 • Awe ni raia wa Tanzania.
 • Awe Mkazi  wa kawaida  wa Kata husika anayoombea.
 • Awe na   umri usiopungua  miaka 18.
 • Awe na elimu ya kuanzia Kidato cha Nne na ajue kusoma na kuandika .
 • Awe na umahiri  katika Matumizi  ya Kompyuta.
 • Asiwe Kiongozi  au Kada  wa chama cha Siasa.
 • Awe mwadilifu na mwaminifu.
 • Waombaji  waliowahi kufanya kazi kiustadi  katika zoezi  la uandikishaji  na wanazo sifa zilizotajwa  hapo juu watapewa  kipaumbele.
 • Sifa za Mwombaji  wa nafasi  ya Mwandishi Msaidizi
 • Awe ni raia wa Tanzania.
 • Awe Mkazi  wa kawaida  wa Kata husika anayoombea.
 • Awe na   umri usiopungua  miaka 18.
 • Awe na elimu ya kuanzia Kidato cha Nne na ajue kusoma na kuandika .
 • Awe na umahiri  katika Matumizi  ya Kompyuta.
 • Asiwe Kiongozi  au Kada  wa chama cha Siasa.
 • Awe mwadilifu na mwaminifu.
 • Waombaji  waliowahi kufanya kazi kiustadi  katika zoezi  la uandikishaji  na wanazo sifa zilizotajwa  hapo juu watapewa  kipaumbele.
 • Majukumu ya Mwandishi Msaidizi  na BVR  Kit Operators
 •  
 • Kuhakikisha kuwa kituo kinafunguliwa  kwa wakati  na kuanza uandikishaji  kwa muda uliopangwa  ambao kwa mujibu wa maelekezo ya Tume  ni saa 2;00 asubuhi hadi saa 12;00 jioni.
 • Kuabandika bango la Kituo cha Kuandikisha  Wapiga kura na mabango mengine  yaliyotolewa na Tume kwa ajili ya kituo cha  uandikishaji.
 • Kuhakikisha Vifaa muhimu vya kituo vinakuwepo  katika kituo  cha kuandikisha  wapiga kura.
 • Kuwepo kituoni muda wote wa kazi  hata kama hakuna wapiga kura wanaokuja kujiandikisha  au kuboresha taarifa zao.
 • Kusimamia ujazaji wa fomu   za Mwombaji (Mpiga Kura)ili kuepusha makosa.
 • Kuingiza taarifa za Mpiga kura kwenye Mfumo  wa Uandikishaji .
 • Kuhakikisha kuwa Wapiga kura waliokuja kituoni  kabla ya saa 12;00 na kupanga foleni wanaandikishwa wote  isipokuwa kama wanakuwa wengi  wataorodheshwa majina na kuwapanga kuanza nao siku inayofuata.
 • Kuhakikisha kuwa baada ya uandikishaji  wa siku kukamilika, taarifa ya Wapiga kura walioandikishwa  kwa siku hiyo  inaandaliwa na kutunzwa  kwa Lengo la kumkabidhi Afisa Mwandikishaji Msaidizi ngazi ya Kata.
 • Kuhakikisha kuwa Vifaa na nyaraka za uandikishaji vinatunzwa  vizuri  kipindi chote cha zoezi na kuvikabidhi  kwa Afisa Mwandishaji  vikiwa  katika ubora wake.
 • Majukumu mengine  atakayopangiwa  na Afisa Mwandikishaji  au Afisa Mwandikishaji Msaidizi.

 

 • Mambo ya Kuzingatia  wakati wa kutuma maombi

 

 • Mwombaji Lazima aainishe  kazi anayoomba  kati ya Mwandishi Msaidizi au BVR Kit Operator
 • Waombaji waambatanishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani  na namba za simu  za kuaminika  pamoja na majina  ya wadhamini(Referees)wawili  pamoja na picha tatu (Pasport size za hivi karibuni.
 • Maombi yote yatapaswa kuambatana na nakala  za vyeti  vya kitaaluma  na kitaalamu.
 • Mwombaji ambaye ni Mtumishi wa Umma atapaswa kupitisha maombi  kwa mwajiri wake,Mwombaji ambae  si Mtumishi  wa Umma  maombi yake yapitie kwa Mtendaji wa Kata  husika  anayaoomba kufanya kazi.
 • Mwisho wa Kutuma maombi  ni tarehe 26/04/2020
 • Maombi yote yatumwe  kupitia anuani  ifuatayo;
 • AFISA MWANDIKISHAJI,
 • JIMBO LA PERAMIHO,
 • S.L.P 995,
 • SONGEA
 • TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA
Sharing is Caring! Click on the Icons Below and Share


      Method of Application

Submit your CV and Application on Company Website : Click Here

Closing Date : 26th April, 2020.


Dont Miss Latest Jobs In Tanzania. Subscribe Today. CLICK HERE

Apply for this Job