11 Feb 2019

Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa Jobs in Tanzania : Mtendaji Wa Kijiji Daraja La III x5

Welcome to JobwebTanzania.com. This website helps you to achieve your career dream by linking you to vacancies from Top Companies in Tanzania. Job Seekers are also exposed to best articles for career growth and development. Click Here to Subscribe for Job Alerts We strongly advise graduates not to pay money before getting a Job. Report fraudulent jobs to [email protected]


Ofisi Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa

Tangazo La Nafasi Za Kazi
Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa Anawatangazia Wananchi Wote Wenye Sifa Na Nia Ya Kufanya Kazi Katika Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa Kwa Nafasi Mbalimbali Kama Ifuatavyo;
5 Mtendaji Wa Kijiji Daraja La III

SIFA ZA MWOMBAJI:
• Awe amehitimu Kidato cha Nne au sita
• Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo:-Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MAJUKUMU YAKE:
• Kuwa Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
• Kusimamia ulinzi na usalama wa Raia na Mali zao
• Kuratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
• Kuwa katibu wa mikutano yote ya Halmashauri ya kijiji.
• Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
• Kuandaa taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
• Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalamu katika kijiji.
• Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji.
• Mwenyekiti wa kikao cha Wataalamu waliopo katika kijiji.
• Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
• Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji
• Baruapepe: [email protected]
• Tovuti: www.iringadc.go.tz
• Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
NGAZI YA MSHAHARA TGS B

Sharing is Caring! Click on the Icons Below and Share

How to Apply

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA: • Barua za Maombi ziambatishwe na nakala za Vyeti vya Elimu, Taaluma na Cheti cha kuzaliwa, • Mwombaji aambatishe Picha mbili za rangi(Passport Size) za hivi karibuni • Waombaji wa nafasi ya Udereva waambatishe Leseni ya Udereva. • Kwa wale waliosoma Nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka (TCU au NECTA kulingana na ngazi ya Cheti) • Maombi yaambatishwe na Maelezo binafsi (CV). • Umri wa waombaji usizidi miaka 45 • Mwisho wa kupokea maombi hayo ni tarehe 22.02.2019 saa 09:30 Alasiri. • Barua zote za Maombi ziandikwe kwa mkono , na zitumwe kwa anuani ifuatayo;- Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya, S. L. P. 108, IRINGA IMETOLEWA NA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA.


Dont Miss Latest Jobs In Tanzania. Subscribe Today. CLICK HERE

Apply for this Job