11 Feb 2019

Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa Jobs in Tanzania : Katibu Muhtasi Daraja La III

Welcome to JobwebTanzania.com. This website helps you to achieve your career dream by linking you to vacancies from Top Companies in Tanzania. Job Seekers are also exposed to best articles for career growth and development. Click Here to Subscribe for Job Alerts We strongly advise graduates not to pay money before getting a Job. Report fraudulent jobs to [email protected]


Ofisi Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa

Tangazo La Nafasi Za Kazi
Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa Anawatangazia Wananchi Wote Wenye Sifa Na Nia Ya Kufanya Kazi Katika Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa Kwa Nafasi Mbalimbali Kama Ifuatavyo;
Katibu Muhtasi Daraja La III

SIFA ZA MWOMBAJI:
• Awe amehitimu Kidato cha Nne
• Awe amehudhuria Mafunzo ya Uhazili na Kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu.
• Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno themanini (80) kwa dakika moja.
• Awe amepata Mafunzo ya Kompyuta kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na Kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet, Email na Publisher

MAJUKUMU YAKAZI:
• Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
• Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
• Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za Vikao, safari za Mkuu wake na Ratiba ya kazi zingine zilizopangwa
• kutekelezwa katika ofisi anayofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
• Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
• Kusaidia kufikisha maelezo ya Mkuu wake wa kazi kwa Wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na Wasaidizi hao.
• Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo, na kukusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
• Kutekeleza kazi zote atakazopangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
NGAZI YA MSHAHARA TGS B

Sharing is Caring! Click on the Icons Below and Share

How to Apply

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA: • Barua za Maombi ziambatishwe na nakala za Vyeti vya Elimu, Taaluma na Cheti cha kuzaliwa, • Mwombaji aambatishe Picha mbili za rangi(Passport Size) za hivi karibuni • Waombaji wa nafasi ya Udereva waambatishe Leseni ya Udereva. • Kwa wale waliosoma Nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka (TCU au NECTA kulingana na ngazi ya Cheti) • Maombi yaambatishwe na Maelezo binafsi (CV). • Umri wa waombaji usizidi miaka 45 • Mwisho wa kupokea maombi hayo ni tarehe 22.02.2019 saa 09:30 Alasiri. • Barua zote za Maombi ziandikwe kwa mkono , na zitumwe kwa anuani ifuatayo;- Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya, S. L. P. 108, IRINGA IMETOLEWA NA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA.


Dont Miss Latest Jobs In Tanzania. Subscribe Today. CLICK HERE

Apply for this Job