9 Feb 2019

Benjamin William Mkapa Jobs in Tanzania : Wateknolojia wasaidizi mionzi x21

Welcome to Jobweb Tanzania. This website helps you to achieve your career dream by linking you to vacancies from Top Companies in Tanzania. Job Seekers are also exposed to best articles for career growth and development. Click here to subscribe for job alerts We strongly advise graduates not to pay money before getting a Job. Report fraudulent jobs to [email protected]


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin William Mkapa, inatekeleza Mradi wa kuimarisha Mifumo Endelevu ya Afya (RSSH) kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund).

Mradi huu una lengo la kuimarisha huduma za afya ngazi za vituo katika mikoa kumi (10) iliyopewa kipaumbele na mradi huu ambayo ni; Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Geita, Kagera, Katavi, Tabora, Dodoma na Kigoma. Kupitia mradi huu, jumla ya wataalamu 281 wamepangwa kuajiriwa kwa kipindi cha mwaka 2018
– 2020 na kupangiwa kufanya kazi ndani ya mikoa tajwa hapo juu. Ili kukamilisha ujazaji wa nafasi za wataalamu zilizobakia wazi, Taasisi ya Mkapa inapenda kutangaza nafasi wazi 90 za wataalamu wa afya. nin

Nafasi hizi ni kwa ajili ya wataalamu waliosomea fani za:.
21 Wateknolojia wasaidizi mionzi

Sifa za waombaji;
• Waliohitimu mafunzo kutoka katika vyuo vinavyotambulika na Serikali.
• Wataalamu wenye vyeti kamili vya mafunzo ya fani walizosomea.
• Wataalamu wenye leseni hai kutoka katika mamlaka za usajili kwa fani zinazotakiwa kufanya usajili kabla ya kuanza kufanya kazi.
• Mtanzania mwenye umri chini ya Miaka 45. Wataalamu ambao wameajiriwa katika ajira za serikali na za kidini,
• hawatakiwi kuomba ajira hizi.

Maombi yote yaambatanishwe na:
• Barua ya maombi ya kazi ikieleza Mikoa mitatu ambayo muombaji angependa kupangiwa kufanya kazi katika moja ya Halmashauri zake.
• Nakala ya cheti cha Taaluma.
• Cheti cha kidato cha 4 na 6 kama kipo.
• Picha mbilmli (2)
• Passport size na maelezo binafsi (CV), ikionyesha umri, anuani kamili na namba ya simu ya kiganjani, pamoja na anuani/ namba ya kiganjani ya wadhamini wako wasiopungua wawili.
• Nakala zote za vyeti ziwe zimepitishwa na mwanasheria ili kuthibitisha kama ni nakala halisi ya cheti cha mwombaji.

Sharing is Caring! Click on the Icons Below and Share


      Method of Application

Maombi yote yatumwe kwa: Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa, kwa sanduku la Posta 76274 Dar Es Salaam au kwa barua pepe [email protected]  . Mwisho wa kupokea maombi ya kazi itakuwa tarehe 28 Februari 2019. Tangazo hili la kazi linapatikana pia katika tovuti ya Taasisi ya Mkapa: www.mkapafoundation.or.tz . NB: Majibu yatatolewa kwa watakaofanikiwa tu. IMETOLEWA NA Afisa Mtendaji Mkuu Taasisi ya Benjamin William Mkapa


Dont Miss Latest Jobs In Tanzania. Subscribe Today. CLICK HERE

Apply for this Job